Mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameachana na mpenzi wake raia wa Urusi, Irina Shayk.
Wawili hao wamedumu kwa kipindi cha miaka mitano.
“Tunathibitisha kuwa Irina Shayk amevunja uhusiano wake na Cristiano Ronaldo,” mwakilishi wake aliiambia Page Six jana.
Tetesi za kuachana kwa mastaa hao zilianza kuvuma baada ya Shayk
kutoonekana akiwa na Ronaldo kwenye tuzo FIFA Ballon d’Or jijini Zurich
Jumatatu.
Badala yake mchezaji huyo alisindikizwa na mama yake, Maria Dolores
dos Santos Aveiro, na mwanae Cristiano Jr aliyezaa na mwanamke
asiyejulikana.
Post a Comment