Mrembo na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu amefunguka na
kudai kuwa mwigizaji Van Vicker wa Ghana, alichania kwa kiasi flani, kupelekea aachane na aliekuwa mpenzi wake, Diamond.
Kwamujibu wa GPL,akizungumzia sababu za kumwagana na Diamond, alisema pamoja na sababu nyingine, Van Vicker alihusika kuwafanya wamwagane na mpenzi wake huyo waliyedumu kwenye penzi zito lililokuwa gumzo kila kona ya Bongo.
“Kuna vitu vingi vimechangia lakini Van pia amechangia, alianza ku-like picha zangu, nikamwambia Dai (Diamond), akaniambia achana naye, baadaye tulibadilishana namba, tukawa tunawasiliana.
“Ilipofika wakati amenitaka tufanye kazi pamoja, nilipomwambia Diamond ndiyo matatizo yalipoanzia hadi kufikia hatua ya kuachana,” aliweka nukta Wema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment