Siku chache baada ya kuripotiwa kuwa ni
mjamzito, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameibuka na kufunguka
kuwa, aachwe azae kwani umri unazidi kuyoyoma.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Aunt
alisema watu wamekuwa wakizungumza sana kuhusu ujauzito wake lakini
kikubwa ni kwamba ameupata akiwa na umri sahihi na wala siyo chini ya
miaka 18. “Najua watu wengi wanazungumza kuhusu mimi na ujauzito wangu
lakini mimi sijaona tatizo na tena siko chini ya umri wa miaka 18 sijui
kama kuna tatizo lolote nikipata mtoto na hivyo kama mimba ipo watu
wasubiri , ” alisema Aunt ambaye amekuwa mzito kuanika umri wake
hadharani.
Aunt ambaye aliolewa mwaka 2012 na
Sunday Demonte anayedaiwa kusota nyuma ya nondo huko Dubai kwa msala wa
madawa ya kulevya, kwa sasa anadaiwa kubanjuka kimapenzi na dansa wa
Nasibu Abdul ‘ Diamond ’ , Moze Iyobo . Hata hivyo, mimba hiyo ya Aunt
haijajulikana kama ni ya Iyobo au mwanaume mwingine maana wawili hao
wamekuwa wakichenga kuizungumzia.
Post a Comment